map | search | help | download | contact us | françaisfrançais
ltbp.org : what is LTBP? : overview
 
 What is LTBP?
Overview
Participants
Regional Offices
 Features:
Calendar
Photo Gallery
Publications
 Programmes:
Biodiversity
Environmental Edu.
Fishing Practices
Geogr. Info. Syst.
Pollution
Sedimentation
Socio-economics
Training
 Processes:
Legal Convention
Strat. Action Prog.
 Management:
Reg. Co-ordination
 Projects:
Nyanza Course
Uvira Renovations
World Environ. Day
 Administration:
 Project Resources
   
Mradi
Miongoni mwa malengo makuu ya mradi ni uanzishaji wa mpango wa kanda unaoweza kujiendesha wa usimamizi wa udhibiti wa uchafuzi wa mazingira, hifadhi na matengenezo ya bioanuwai katika Ziwa Tanganyika. Msingi wa mradi utatokana na matokeo ya tafiti za fani nyingi mbalimbali zinazolenga kuboresha uelewa wa masuala changamani ya kisayansi, kiufundi, kisheria kijamii na kiuchumi yanayohusu hifadhi ya ziwa na mazingira yanayolizunguka.

Tafiti hizi zimegawanyika katika makundi madogo matano, ambayo pengine huingiliana kutokana na hali halisi inayokabiliwa. Makundi hayo ni bioanuwai, uchafuzi wa mazingira, ushapishaji, uchumi-jamii na elimu ya mazingira. Tafiti za bioanuwai zinakusudia kutafuta ni spishi zipi, na spishi za mazingira gani uhai wake unatishiwa. Tafiti juu ya uchafufuzi wa mazingira zitatafuta vyanzo vya uchafu, na pia zitatathmini madhara ya uchafu na kutafuta hatua za kuzuia kuenea kwa uchafu. Tafiti za ushapishaji zitahusu kujengeka kwa miamba na udongo kutokana na kulundikana na kugandamana kwa udongo na takataka. Tafiti hizo zitachunguza mwenendo na athari ya udongo unaoingia ziwani. Tafiti za uchumi-jamii na elimu ya mazingira ni programu mbili zilizofungamana zinazolenga kuinua ufahamu wa masuala muhimu ya kimazingira miongoni mwa vikundi vya watumiaji wa mazingira.

Programu hizi zitasaidia ufasiri wa tafiti za kisayansi katika mambo na mipango inayoweza kutekelezwa katika maeneo fulani ambamo wakazi wake wanaweza kuchukua dhima kubwa zaidi katika hifadhi na maendeleo. Chini ya mada hizi vilevile zipo tafiti juu ya uvuvi na kilimo, ustahilifu wa maeneo kwa ajili ya kuanzisha hifadhi za taifa za chini ya maji, uhusiano wa mifumo ya kisheria ya miliki ya ardhi, hifadhi ya ziwa na mahitaji ya kimaendeleo zinazozingatia matatizo yote yanayohusiana na masafa marefu na mawasiliano duni yaliyopo.

Chini ya uratibu kutoka makao makuu ya mradi jijini Dar es Salaam, kazi hufanywa na timu za wataalam walioazimwa kutoka idara za serikali, vyuo vikuu, asasi za utafiti na mashirika yasiyo ya kiserikali. Wataalam hawa kufanya kazi kwa kushirikiana na wataalamu wa kimataifa wa fani zao na pia wanajumuia ambao maisha yao yanalitegemea sana ziwa. Wakati wa kuelekea mwishoni mwa mradi, inatarajiwa kuwa asasi zilizomo kwenye kanda hii zitakuwa zimejijengea uwezo wa kuendeleza kazi ya ufuatiliaji na ushauri unaohitajika kuhakikisha kuwepo kwa usimamizi wa mazingira wa muda mrefu wa eneo la ziwa.

Mwitikio imara wa serikali za nchi nne zinazolizunguka ziwa (Burundi, Tanzania, Zambia na Zaire) tayari umehakikishwa. Nchi hizi zinaelewa fika ukubwa wa umuhimu wa kazi iliyo mbele yao na hali kadhalika haja ya kuzingatia sheria zinazohusu matumizi ya ziwa. Sasa ni jukumu la mradi kuamisha mitazamo inayolingana na hii miongoni mwa wakazi wa eneo la vyanzo vya maji vya ziwa na kuanzisha miundombinu itakayowawezesha kusimamia kwa ufanisi maisha yao ya baadaye.

Mradi utachukua miaka mitano kuanzia mwaka 1995 hadi mwaka 2000 na unafadhiliwa na Shirika la Kimataifa linalohusu Mazingira kupitia Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP). Mradi unatekelezwa kupitia Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Huduma za Miradi na Taasisi ya Maliasili kwa kushirikiana na mashirika mawili ya utafiti ya nchini Uingereza, yaani MRAG Ltd na Taasisi ya Ekolojia ya Maji ya Baridi.

 
|| Home ||
 
Back Previous: Page 5 of 7  Next: Page 7 of 7 Next

© 1998 - 2002 Lake Tanganyika Biodiversity Project - UNDP/GEF/RAF/92/G32

Authors | Feedback