map | search | help | download | contact us | françaisfrançais
ltbp.org : what is LTBP? : overview
 
 What is LTBP?
Overview
Participants
Regional Offices
 Features:
Calendar
Photo Gallery
Publications
 Programmes:
Biodiversity
Environmental Edu.
Fishing Practices
Geogr. Info. Syst.
Pollution
Sedimentation
Socio-economics
Training
 Processes:
Legal Convention
Strat. Action Prog.
 Management:
Reg. Co-ordination
 Projects:
Nyanza Course
Uvira Renovations
World Environ. Day
 Administration:
 Project Resources
   
Wakazi wa Eneo
Idadi ya wakazi wa eneo la vyanzo vya maji vya Ziwa Tanganyika inakisiwa kuwa kati ya watu milioni 7 hadi 10 na idadi hii inaongezeka kwa haraka. Idadi kubwa zaidi ya watu wanaoishi kwenye eneo la vyanzo vya maji vya ziwa wanategemea kilimo na uvuvi kwa ajili ya chakula chao na mapato. Shughuli za viwanda na uchafuzi wa mazingira katika eneo la vyanzo vya maji vya ziwa vipo katika sehemu fulani fulani chache maalum kutokana na maendeleo duni ya bonde.

Wakazi wa eneo hili wanalithamini ziwa kwa sababu kadhaa: kama chanzo cha samaki, njia ya usafiri, chanzo cha maji ya kunywa na kuoga, kuoshea vyombo na matumizi mengine ya nyumbani na kama hifadhi ya maji kutoka kwenye mito mbalimbali. Kwa hali hii watu wengi hulitambua ziwa kama chombo muhimu kwa uhai wao. Kwa bahati mbaya mitazamo ya kimapokeo na usimamizi wa mali inayotokana na ardhi na maji na pia njia zinazotumika kuondosha takataka, haziwezi tena kuhimili kwa vile haziwezi kwenda sambamba na kasi ya ongezeko la msongamano wa watu. Kwa kawaida mawasiliano na upatikanaji wa huduma za umma kandokando mwa ziwa ni duni. Matatizo haya yanamaanisha kuwa uamuzi wowote wa serikali kuu juu ya matumizi ya bonde la Ziwa utakuwa mgumu kutekelezwa na jumuiya za kandoni mwa ziwa.

 
|| Home ||
 
Back Previous: Page 3 of 7  Next: Page 5 of 7 Next

© 1998 - 2002 Lake Tanganyika Biodiversity Project - UNDP/GEF/RAF/92/G32

Authors | Feedback